Yanga yaibomoa Azam FC, yampa miaka miwili Gadiel Michael
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam
Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga SC nao wameibomoa Azam FC ambayo hivi karibuni iliwanyang' anya wachezaji wake watatu iliotaka kuingia nao mikataba.
Yanga imemnasa beki wa kushoto wa Azam na timu ya taifa, Taifa Stars, Gadiel Michael kwa kumpa kandarasi ya miaka miwili.
Taarifa zenye uhakika kabisa zinasema mchezaji huyo ameridhia kutua Yanga lakini atalazimika kufanya siri ili mkataba wake umalizike na ndiyo ajiunge na Yanga.
Mkataba wa Gadiel unaishia Desemba mwaka huu hivyo atalazimika kuitumikia Azam katika mzunguko wa kwanza, na mzunguko wa pili ataanza kuitumikia Azam, Azam FC nao wameanza kuachana na wachezaji wake na inasemekana mishahara mikubwa inawashinda kwa sasa