RASHID MANDAWA HAENDI KOKOTE
Na Albert Babu. Morogoro
Uongozi wa timu ya Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro, umesema mshambulizi wake Rashid Mandawa "Chididebe" haendi kokote na wamepanga kumwongezea mkataba mpya.
Akizungumza na Mambo Uwanjani, Afisa Habari wa Mtibwa Sugar, Tobias Kifaru amesema Mandawa hawezi kuihama Mtibwa kwakuwa bado wanamuhitaji.
Ameongeza kuwa tetesi za usajili kwa nyakati hizi ndiyo wakati wake lakini ukweli unabaki palepale, anasema Mandawa ni mshambuliaji mahiri hivyo haiwezi kuwa rahisi kumwachia aende.
Mtibwa Sugar ilimchukua Mandawa kutoka Stand United na tangu atue hapo ameweza kuisaidia timu hiyo na kuendelea kusalia katika nafasi za juu, pia Mtibwa imesema itaendelea kuwabakiza karibu nyota wake wote hasa baada ya beki wake Ally Shomari kujiunga na Simba ya Dar es Salaam