Ajibu sasa rasmi Yanga, mkataba wake wawekwa hadharani
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Yanga SC imeamua kuweka hadharani usajili wa mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajibu Migomba 'Kadabla' na imeuanika mkataba wake wa miaka miwili.
Uongozi wa Yanga kupitia kwa katibu mkuu wake Charles Boniface Mkwasa aliwaambia Wanayanga kuwa wameshamslizana na Ajibu na kinachosubiriwa kwa sasa ni kumalizika kwa mkataba wake na Simba mwishoni mwa mwezi huu.
Ajibu aligomea kuongeza mkataba mpya na Simba lakini akalainika kusaini mkataba wa miaka miwili Jangwani na inaaminika kuwa ana mapenzi makubwa na Yanga na sasa atavaa uzi wa kijani na njano, Ajibu aliibuliwa na Simba akipitia timu ya vijana, Simba B