Kaburu kujiuzuru umakamu wa Rais Simba
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Kwa mujibu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) limesisitiza kuwa ili uchaguzi mkuu wa TFF ufanyike ni lazima wagombea wote watambue kuwa endapo uchaguzi utaisha na ukapata viongozi wake ni lazima wasalie na nafasi moja tu.
Mohamed Kiganja kaimu katibu mkuu wa Baraza hilo alisisitiza masharti hayo yafanye kazi, hiyo inakuja kufuatia viongozi wa Shirikisho hilo kuwa na nafasi ya madaraka zaidi ya moja.
Makamu wa Rais wa Simba Geofrey Nyange "Kaburu" anayegombea umakamu wa rais wa TFF yuko hatarini kujiuzuru nafasi yake ya umakamu wa rais katika klabu yake ya Simba endapo atachaguliwa.
Siyo Kaburu peke yake hata Jamal Malinzi ambaye ni rais wa Shirikisho hilo, atalazimika kuachia ngazi nafasi ya mwenyekiti wa chama cha soka mkoani Kagera kama atafanikiwa kutetea kiti chake