NGOMA ASAINI POLOKWANE CITY MIAKA MITATU
Na Mwandishi Wetu. Afrika Kusini.
Hatimaye maisha ya mshambulizi wa kimataifa raia wa Zimbabwe katika klabu ya Yanga SC ya Tanzania yamefikia tamati baada ya leo kusaini kandarasi ya miaka mitatu kwa klabu ya Polokwane City inayoshiriki Ligi Kuu ya Absa.
Ngoma amemaliza mkataba wake wa miaka miwili na Yanga na alikuwa katika mvutano mkali na uongozi wa timu hiyo, mapema leo katibu mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa aliwahakikishia Wanayanga kuwa wamejipanga kumuongezea mkataba straika huyo aliyekuwa katika kiwango kizuri.
Ngoma amefuzu vipimo vyake vya afya na Polokwane City wakaamua kumpa mkataba wa miaka mitatu, akiwa na Yanga, Ngoma aliipa ubingwa wa bara mara mbili mfululizo, kombe la FA, na kuiwezesha kufuzu hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika