Uingereza yasikitishwa na Tanzania kumpoka mtaa Wanyama
Vyombo vya habari tena vile vikubwa nchini Uingereza vimelaani vikali kitendo cha Tanzania kumpora mtaa mwanasoka wa kimataifa anayeichezea klabu kubwa duniani ya Tottenham Hotspurs inayoshiriki Ligi Kuu ya Premia, Victor Wanyama.
Wanyama ambaye ni raia wa Kenya ana uhuru wa kuchagua nchi yoyote kwenda kupumzika na katika mapumziko yake akaichagua Tanzania katika jiji la Dar es Salaam kama sehemu yake ya mapumziko baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya Uingereza.
Akiwa jijini Dar es Salaam, Wanyama alitembelea Ubungo Shekilango kwenda kutazama Ndondo Cup ambapo pia alikutana na mbunge wa Ubungo, Boniface Jacob na kumpa mtaa, Wanyama alipewa mtaa wa Viwandani na kuitwa jina lake Victor Wanyama Street.
Lakini kesho yake uongozi wa serikali ya mtaa huo ukang' oa bango lililowekwa likielekeza mtaa huo, pia serikali ya mtaa huo ikasema wameamua kufuta jina la mtaa kwa maana hazikufuatwa taratibu.
Uingereza imelaani kitendo ikisema haijamtendea haki Wanyama na itambue kuwa mwanasoka huyo ni mkubwa na ndio maana amesajiliwa na kulipwa mamilioni ya shilingi na klabu hiyo