Yassar awa mshindi wa tatu michuano ya draft Tabata
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Kijana aliyefahamika kwa jina la Yassar usiku huu amefanikiwa kupata ushindi wa tatu katika michuano ya kumtafuta bingwa wa draft Tabata Mtambani baada ya kumfunga bao 1-0 mpinzania wake Mroka.
Ushindi huo haukuja bure ni baada ya kucheza michezo mitatu na miwili walitoka suluhu huku wa mwisho aliweza kuibuka na ushindi, Yassar alifikia kucheza mechi hiyo ya mshindi wa tatu baada ya kuondoshwa kwenye nusu fainali na mpinzani wake Charles Chinguile.
Yassar alifungwa bao 1-0, wakati Mroka naye alifungwa na Michael Mtanga pia bao 1-0, fainali itapigwa kesho kati ya Charles na Michael na bingwa atapata kuku jogoo.