Nyamlani ashituka, ajitoa mbio za urais TFF

Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam

Mgombea wa nafasi ya Urais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania, (TFF) Athuman Nyamlani amejitoa katika kinyang' anyiro hicho leo.

Kwa mujibu wa Afisa habari wa TFF, Alfred Lucas amesema Nyamlani amewaandikia barua ya kujitoa kwenye mbio za kuwania Urais wa Shirikisho hilo na hakuweza kuwapa sababu zilizopelekea kujitoa kwake.

Lakini kwa taarifa ambazo Mambo Uwanjani inazo inafahamu fika kuwa Nyamlani ameshitukia hujuma zinazofanywa na mmoja wa washindani wake wakuu (Jina tunalo).

Kujitoa kwa Nyamlani sasa kunaongeza joto kwa washiriki waliosalia kwenye mbio hizo, Nyamlani aliwahi kuwa makamu wa kwanza wa Rais wa Shirikisho hilo likiwa chini ya Leodegar Tenga

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA