Taifa Stars yaapa kuilaza Malawi
Na Exipedito Mataruma. Afrika Kusini.
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo inajitupa uwanjani hapa Afrika Kusini kukwaruzana na timu ya taifa ya Malawi mchezo wa michuano ya COSAFA kundi A.
Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga amesema vijana wake wapo tayari kwa mchezo huo na wataweza kuibuka na ushindi katika mchezo huo, michuano hiyo inaanza leo na michuano hiyo inajumlisha karibu timu ,13.
Tanzania, Angola, Mauritius na Malawi zenyewe zimepangwa kundi A wakati kundi B lina timu za Shelisheli, Msumbiji, Madagascar na Zimbabwe, timu za Afrika Kusini, Zambia, Botswana, Namibia na Lesotho zitacheza mechi za mtoano