Ni vita ya Tanzania na Angola leo
Na Exipedito Mataruma. Afrika Kusini.
Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, jioni ya leo kitashuka uwanjani kwa mara ya pili kukwaruzana na Angola katika mchezo wa michuano ya kombe la COSAFA Castle Cup.
Tanzania inahitaji ushindi katika mchezo huo ili iweze kutinga robo fainali ya michuano hiyo inayoshirikisha mataifa 13, Tanzania ikishiriki kama nchi mwalikwa, ilianza vema katika fainali hizo baada ya kuilaza Malawi mabao 2-0.
Mabao yote ya Tanzania yalifungwa na winga wake Shiza Kichuya, kuelekea katika mchezo wa jioni, kocha wa Tanzania Salum Mayanga amesema vijana wake wapo tayari kwa mchezo huo na amewaahidi Watanzania zawadi nzuri ya sikukuu ya Iddi El Fitr