Ronaldo siyo kwenye soka peke yake, apiga hat trik ya watoto
Mshambuliaji wa kutumainiwa wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo amebahatika kupata watoto wawili kwa mpigo baada ya mkewe kujifungua kwa mpigo.
Sasa Ronaldo anakuwa baba wa watoto watatu na kumfanya adhihirishe makali yake kuwa yeye siyo kwenye mchezo wa soka pekee hata kunako familia anatisha.
Ronaldo ametoka kushiriki kombe la mabara ambapo timu yake ya Ureno imeondoshwa kwa mikwaju ya penalti na Chile, mwanasoka huyo bora wa dunia ametishia kuihama Real Madrid ili kukwepa kodi Hispania