YANGA MAFIA, WAMSHUSHA NGOMA USIKU HUU
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam.
Yanga jeuri bwana, usiku huu wamemshusha mshambuliaji wao Mzimbabwe Donald Ngoma anayedaiwa kumwaga wino katika timu ya Polokwane City ya Afrika Kusini kwa mkataba wa miaka mitatu.
Awali katibu mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa aliwahakikishia Wanayanga kwamba ni lazima wampe mkataba mpya mshambulizi wao Donald Ngoma.
Lakini jioni ya leo kumezuka taarifa kuwa mshambuliaji huyo amesaini mkataba wa miaka mitatu katika timu ya Polokwane City ya bondeni kwa Jacob Zuma, Mambo Uwanjani inajulishwa usiku huu Ngoma ametua Airport ya Dar es Salaam tayari kwa kusaini mkataba mpya.
Huo ni umafia mkubwa kuwahi kufanywa na mabingwa hao kwani Ngoma pia alitajwa kujiunga na Simba ambao ni mahasimu wa Yanga