STARS YAKOMAA KILELENI SAUZI
Na Exipeditor Mataruma. Afrika Kusini.
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeilazimisha sare tasa 0-0 dhidi ya Angola mchezo wa kundi A michuano ya Cosafa Castle Cup Uwanja wa Royal Bafokeng mjini Rustenburg, Afrika Kusini.
Mechi hiyo ilipigwa usiku kuanzia saa 2:30 ilishuhudiwa kiungo wake Muzamiru Yassin Selembe akiibuka Man of the Match akionyesha kiwango kikubwa.
Kwa maana hiyo Stars imefikisha pointi 4 ikiongoza kundi A kwa wingi wa mabao dhidi ya Angola ambao nao wana pointi 4 kama Stars ila wao wana bao moja wakati Stars inayo mawili, keshokutwa Stars itacheza na Mauritius mechi ikipigwa jioni