Kagera Sugar wamefoji mkataba wa Mbaraka Yusuf

Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam

Inadaiwa kuwa timu ya Kagera Sugar ya mkoani Kagera imefoji mkataba wa aliyekuwa mchezaji wake Mbaraka Yusuf Abeid ambaye kwa sasa ni mali ya Azam FC.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Azam FC leo baada ya kulalamikia kitendo kinachofanywa na viongozi wa Kagera Sugar kudai Mbaraka Yusuf ni mchezaji wao na wana mkataba naye wa miaka miwili si kweli.

Azam wanadai wamezungumza vizuri na Mbaraka na kugundua kuwa mkataba wake alioingia na Kagera Sugar ni wa mwaka mmoja ambao tayari umemalizika, leo Azam pamoja na Mbaraka waliongozana hadi TFF na kukuta mikataba miwili mmoja ukiwa umefojiwa ambao unaonyesha Mbaraka amesaini miaka mitatu.

Azam wanaituhumu Kagera kwa kuwafanyia kauzibe juu ya kumpata Mbaraka lakini wamesema haki itendeke kwani Mbaraka ni mali yao kihalali na ataitumikia Azam msimu ujao

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA