MAVUGO APATA TIMU RWANDA

Na Saida Salum. Dar es Salaam

Mshambuliaji wa kimataifa wa Klabu ya Simba, Laudit Mavugo raia wa Burundi amepata timu nchini Rwanda ambayo iko tayari kumnunua akitokea Simba SC ya Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa moja kutoka nchini Kenya, inasema kuwa Klabu ya AC Kigali ya Rwanda inayoshiriki Ligi Kuu Bara imetenga kumchukua straika huyo na kumpa kandarasi ya miaka miwili.

Mavugo alifunga mabao 10 akiwa Simba iliyomaliza katika nafasi ya pili nyuma ya mabingwa Yanga SC, pia ameiwezesha Simba kutwaa ubingwa wa kombe la FA.

Simba sasa itashiriki michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika mwakani na imeanza kuboresha kikosi chake ambapo tayari nyota mbalimbali wanatajwa kutua wakiwemo John Bocco, Haruna Niyonzima, Donald Ngoma na Waltel Bwalya

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI