Mario Balotelli akubali yaishe, kuongeza mkataba mpya Nice
Mshambuliaji wa zamani wa Inter Milan, Man City na Liverpool, Mario Balotelli raia wa Italia, amekubali yaishe baada ya kukubali kusaini kandarasi nyingine katika klabu yake ya Nice ya Ufaransa inayoshiriki Ligue 1.
Balotelli alikuwa katika mvutano mkubwa na timu yake hiyo aliyoitumikia baada ya kuihama Inter Milan ya Italia ambayo ilimchukua baada ya kuachana na Liverpool.
Hivi karibuni Mario Balotelli alivumishwa kutaka kurejea tena Uingereza ambapo vilabu kadhaa vilitaka kumnyakua ikiwemo Arsenal, pia alipokea ofa mbalimbali barani Ulaya ambapo ilisalia dakika chache kutimka kikosini hapo.
Lakini mabosi wa Nice wakafanya naye mazungumzo ambayo yameweza kumbakisha tena straika huyo mtukutu