HIMID MAO AITOSA YANGA
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Himid Mao Mkami 'Ninja' amesema alishakataa dili ya kujiunga na Yanga kwakuwa bado ana mkataba na Azam FC.
Mao alisema hayo jana akiwa Uwanja wa ndege wa kimataifa Mwl Nyerere tayari kwa safari ya kuelekea nchini Afrika Kusini.
Amesema ni kweli Yanga walimtafuta lakini aliwakatalia waziwazi mpango wao wa kumuhitaji katika kikosi chao, alisema kiungo huyo ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
"Yanga nimewakatalia, kwa sasa siwezi kucheza tena Tanzania endapo nitamaliza mkataba wangu, matarajio yangu ni kucheza nje", amesema Mao ambaye ni mtoto wa kiungo wa zamani wa Pamba FC ya Mwanza.
Hivi karibuni kiungo huyo alienda kufanya majaribio nchini Denmark katika klabu ya Randers inayoshiriki Ligi Kuu, haijajulikana kama alifaulu au amefuzu