OKWI AWAPONZA KABURU, AVEVA

Na Saida Salum. Dar es Salaam

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini, (Takukuru), inawashililia Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva na makamu wake Geofrey Nyange 'Kaburu' kwa tuhuma za kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.

Inadaiwa Aveva na Kaburu kwa pamoja walijipatia pesa za mauzo ya kiungo mshambuliaji wa kimataifa raia wa Uganda Emmanuel Okwi (Pichani kulia) kwa klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia.

Aveva na Kaburu walijipatia zaidi ya dola 300,000 sawa na shilingi milioni 600,000 lakini wakawadanganya Wanasimba na kusema walimuuza kwa kiasi hicho cha pesa ambacho ni dola 300,000.

Hata hivyo fedha hizo za mauzo ziliingizwa kwenye akaunti binafsi na si ya klabu, Takukuru imewahoji viongozi hao kila mmoja na imefahamika kuwa itawafikisha mahakamani, Taasisi hiyo pia inawashikilia viongozi wa TFF, Jamal Malinzi na Celestine Mwesigwa

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA