Nusu fainali ya Draft kupigwa kesho Tabata
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam
Mashindano ya kumsaka bingwa wa mchezo wa Draft kesho yanafikia hatua ya nusu fainali baada ya hii leo kuchezwa mechi nne za robo fainali na washindi wanne kupatikana.
Musa Kibichwa mratibu msaidizi wa michuano hiyo ameuambia mtandao huu kuwa kesho zitachezwa mechi mbili za robo fainali.
Kibichwa amewataja watakaochezwa nusu fainali ni Charles Chinguile 'Paparazi' atakayekipiga na Yassar wakati nusu fainali nyingine ni kati ya Michael Mtanga na Mroka.
Jioni ya leo zilipigwa mechi za robo fainali ambapo Athuman Mpemba alifungwa bao 1-0 na Mroka, Charles Chinguile alimnyanyasa Geofrey Mbawala mabao 2-0 wakati Yassar alimtungua Richard Ted kwa bao 1-0 huku Michael Mtanga alimchapa Cosmas mabao 2-0, bingwa atapata kuku jogoo