Aveva, Kaburu nao kusota rumande
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam.
Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva na makamu wake Geofrey Nyange 'Kaburu' wote wawili wamewekwa rumande Kisutu hadi Julai 13 mwaka huu baada ya kukutwa na makosa ya utakatishaji fedha.
Aveva na Kaburu wakishikiliwa na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mchini (Takukuru) wakidaiwa kutumia vibaya madaraka yao, wawili hao walipandishwa mahakamani leo na kusomewa mashitaka yao.
Wote wawili wamekutwa na hatia na kwakuwa makosa yao hayaruhusu dhamana wametupwa rumande hadi Julai13 mwaka huu watakapopandishwa tena mahakamani.
Kwa mujibu wa Takukuru kupitia kwa Afisa habari wake, Musa Misalaba alisema Aveva na Kaburu wamekutwa na makosa ya utakatishaji fedha na kubwa ni usajili wa mshambuliaji Emmanuel Okwi ambaye aliuzwa kwa klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia na ilidaiwa Simba ilipata zaidi ya milioni 600 lakini vigogo hao wakawadanganya Simba kwa kusema walimuuza kwa milioni 600 wakati si kweli