Raphael Daudi injini mpya Jangwani
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam
Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga SC nao wanazidi kujiimarisha kwa kuziba mapengo yaliyopo, baada ya kuachana na kiungo wake wa Kinyarwanda Haruna Niyonzima, hatimaye Wanajangwani hao wamefikia makubaliano mazuri na kiungo wa Mbeya City, Raphael Daudi.
Daudi kiungo mshambuliaji wa Mbeya City ameonyesha nia ya kujiunga na mabingwa hao wa Bara na inasemekana atasaini mkataba wa miaka miwili, endapo Yanga itamsainisha kiungo huyo atakuwa mchezaji wa pili baada ya Abdallah Shaibu 'Ninja' aliyesajiliwa hivi karibuni.
Pia Wanajangwani hao wanakaribia kumtambulisha kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Ibrahim Ajibu Migomba ambaye naye anadaiwa kusaini mkataba wa miaka miwili