Ronaldo amgomea Perez, anarudi Man Utd
Mshambuliaji wa kimataifa Cristiano Ronaldo raia wa Ureno amekataa kusalia Real Madrid ya Hispania na anataka kurejea Manchester United ya Uingereza.
Licha ya Rais wa Real Madrid Fiorentin Perez kuwahahakishia mashabiki wa timu hiyo kuwa atambakisha Ronaldo ambaye hivi karibuni alihusishwa na kashfa ya ukwepaji kodi.
Ronaldo alituhumiwa na mamlaka za Hispania kuwa alikwepa kodi mwaka 2011 hadi 2014 hivyo anadaiwa jumla ya Dola Milioni 16.5 kitendo kilichopelekea kuamua kutangaza msimamo huo wa kutoweka.
Ronaldo amewaambia rafiki zake kuwa anarejea katika klabu chake cha zamani cha Manchester United kitendo kinachoamsha furaha kwa mashabiki wa Old Trafford kumuona mfalme wa soka duniani akitua kwao