Maelfu wajitokeza kumzika Ally Yanga

Na Paskal Beatus. Shinyanga

Watu mbalimbali wakiwemo wapenzi na mashabiki wa soka wamejitokeza kwa wingi kumzika shabiki maarufu wa klabu ya Yanga na timu ya taifa, Taifa Stars, Ally Mohamed maarufu Ally Yanga aliyezikwa mjini leo mjini Shinyanga.

Ally Yanga alifariki katika ajali ys gari aina Rover Four iliyopinduka na kupondekapondeka vibaya Mpwapwa mkoani Dodoma akiwa kwenye harakati za mbio za Mwenge.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiliwakilishwa na ndugu Mpogolo ambaye ni naibu katibu mkuu wa CCM Tanzania Bara, marehemu Yanga anakumbukwa kwa staili yake ya ushangiliaji iliyomfanya ajulikane.

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli ametuma salamu zake za rambirambi akionyesha kuguswa na msiba huo mzito kwa Wanayanga na wanamichezo kwa ujumla

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA