Waarabu wamfuata Msuva, Sauzi
Na Exipedito Mataruma. Rustenburg.
Matajiri wa Morocco wamempandia ndege winga wa kimataifa wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simon Msuva na kumfuata Afrika Kusini ambapo yupo na timu ya taifa, Taifa Stars ambayo inashiriki michuano ya Cosafa Castle Cup.
Msuva ameivusha Taifa Stars kutinga robo fainali ya kombe la Cosafa likiwa ni goli la kusawazisha dhidi ya Mauritius mchezo uliofanyika jana ukimalizika kwa sare ya 1-1.
Jana vigogo wa timu ya Difaa El Jajida ya Morocco wameamua kutua Afrika Kusini na inasemekana wako tayari sasa kumnasa winga huyo aliye katika kiwango cha juu kwa sasa.
Taarifa ambazo Mambo Uwanjani inazo zinasema kuwa Msuva alikataa mshahara wa Wamorocco hao ambao tayari wameshampata Ramadhan Singano 'Messi' wa Azam FC