Kiemba mbioni kutua Mtibwa Sugar
Na Saida Salum. Morogoro
Kiungo wa zamani wa Kagera Sugar, Yanga, Simba na Taifa Stars, Amri Ramadhan Kiemba anakaribia kujiunga na Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro tayari kabisa kwa ajili ya msimu ujao.
Kiemba aliyekuwa akiichezea Stand United anatarajiwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Mtibwa Sugar timu ambayo imekuwa ikifanya vizuri kwenye Ligi Kuu Bara, miamba hiyo ya mjini Morogoro imethibitisha kumnasa kiungo huyo.
Akiwa Simba, Kiemba aling' ara mno mpaka kuitwa timu ya taifa, Taifa Stars na aliachwa na mabingwa hao wa kombe la FA na kuelekea Shinyanga kujiunga na Stand United ambayo nayo akaachana nayo