Singida United yamnasa mbaya wa Yanga, Azam
Na Saida Salum. Singida
Timu ya Singida United ya mkoani Singida imeendelea kutikisa kwenye usajili baada ya kufanikiwa kumsainisha mkataba wa miaka miwili beki wa kushoto na kulia, Miraji Adam.
Kikosi hicho kilichopanda ligi kuu mwaka huu, imemalizana na mlinzi huyo ambaye amewahi kuzichezea Simba na Coastal Union, Miraji Adam aliyekuwa akiichezea African Lyon iliyotelemka daraja atavaa uzi mpya wa Singida United.
Huu ni usajili wa nane kwa Singida United smbayo imeamua kukiboresha kikosi chake kilichoungana na Njombe mji na Lipuli ya Iringa kucheza Ligi Kuu, Miraji anakumbukwa vema na vilabu vya Yanga na Azam kwani vyote alivitungua