RASMI: YANGA YANAWA MIKONO KWA NIYONZIMA, NJIA NYEUPE MSIMBAZI
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Katibu mkuu wa klabu bingwa ya soka Tanzania Bara, Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa, leo amewaambia Wanayanga kuwa mchezaji wao Haruna Niyonzima wameshindwana katika suala la kuongeza kandarasi nyingine baada ya kumalizika kwa ule wa miaka miwili Julai mwaka huu.
Mkwasa amewaambia Yanga kuwa Niyonzima walikuwa naye kwa misimu sita kwa mafanikio lakini sasa umefika mwisho na wanamruhusu kwa mikono miwili aende huko anakotaka kwenda.
Niyonzima alifunguka jana kuwa bado yeye ni mchezaji wake wa Yanga hadi Julai mwaka huu, lakini bado hajasaini kokote licha ya kuenezwa taarifa kuwa amesaini Simba miaka miwili, Mkwasa amemtakia kheli kiungo huyo raia wa Rwanda aliyetua Yanga akitokea APR ya Rwanda