Sportpesa kusitisha ufadhili wake Kenya
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Kampuni ya michezo ya kubahatisha Sportpesa ya nchini Kenya imetishia kujiondoa ufadhili wake kwa Ligi Kuu ya Kenya (KPL) baada ya serikali ya nchi hiyo kuwaongezea ongezeko la kodi la asilimia 35.
Ofisa wa Sportpesa nchini Kenya, Ronald Karauri amesema kampuni yake itaacha kudhamini Ligi Kuu ya Kenya kwa sababu ya ongezeko hilo la kodi.
Endapo Sportpesa itaacha kufadhili ligi ya Kenya litakuwa anguko kubwa kwa soka la nchi hiyo, Sportpesa inadhamini pia vilabu vya Gor Mahia, AFC Leopards, Nakuru All Stars na Tusker FC.
Naye Afisa wa Kampuni ya Ligi Kuu (KPL) Jack Aduga amesema kujitoa kwa Sportpesa ni pigo kubwa kwao, kampuni hiyo imekuwa ikijitolea mamilioni ya shilingi kufadhili shughuri za soka hivyo kama wataondoka hakuna atakayeweza kubeba mzigo wa soka la Kenya