MALINZI ADAKWA NA TAKUKURU
Na Saida Salum. Dar es Salaam.
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (Takukuru) leo imemkamata Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (Tff) Jamal Malinzi pamoja na katibu mkuu wa Shirikisho hilo Mwesigwa Celestine kwa tuhuma mbalimbali za rushwa.
Ukweli wa kukamatwa kwao haujawekwa wazi licha kwamba Takukuru imethibitisha kuwashikilia watu hao kwa mahojiano zaidi na kama ikithibitika ni kweli wana hatia watafikjshwa mahakamani.
Kukamatwa kwa Malinzi kunatishia nafasi yake ya kurejea tena madarakani katika uchaguzi ujao unaotaraji kufanyika Agosti 12 mwaka huu mjini Dodoma, hata hivyo Mambo Uwanjani imejulishwa kuwa Malinzi anahusika kwa ufujaji wa fedha