Mengi atajwa kuifadhili Yanga
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam
Inaelezwa kuwa mpenzi na mwanachama wa Yanga na mfanyabiashara mkubwa hapa nchini, mmiliki wa makampuni ya IPP, Reginald Abrahamu Mengi anatajwa kutaka kuisaidia timu hiyo baada ya kukimbiwa na aliyekuwa mwenyekiti wake Yusuf Manji.
Mengi na Manji walikuwa hawaivi chungu kimoja na kutajwa kwake kunahusisha mpango wa kujitolea kama mshabiki wa timu hiyo, bado Mambo Uwanjani haijajulishwa kama lini kibopa huyo ataanza kumwaga mamilioni.
Mengi inadaiwa ni mpenzi na mwanachama wa Yanga lakini hakuwahi kujitokeza hata mara moja wakati timu hiyo inafadhiliwa na Yusuf Manji kwakuwa hawakuwa wakielewana ingawa wote ni wamiliki wa makampuni na Mengi ndiye mwenyekiti wao