Tambwe asaini miaka miwili Yanga
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga SC wamezidi kuendelea kuwabakiza nyota wake baada ya usiku huu kuthibitisha kumuongezea mkataba wa miaka miwili mshambuliaji wake Amissi Jocelyin Tambwe.
Tambwe aliyejiunga na mabingwa hao misimu miwili iliyopita akitokea kwa mahasimu Simba, amesaini mkataba mpya leo ambao utamfanya aendelee kusalia hapo hadi mwaka 2019.
Msimu wake wa kwanza Tambwe amekuwa mfungaji bora akifikisha mabao 21 na vilevile bado amekuwa katika kiwango kizuri na kufikia Yanga kunogewa naye na kumuongezea mkataba