Mtanga awa bingwa wa draft Tabata Mtambani
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Hatimaye michuano ya kumsaka bingwa wa mchezo wa draft imemalizika usiku huu huko Tabata kwa kupigwa mchezo mmoja wa fainali ambapo kijana Michael Mtanga alimgalagaza mpinzani wake Charles Chinguile kwa bao 1-0.
Fainali hiyo haikuwa nyepesi kwa Michael Mtanga, kwani ilimchukua raundi ya pili kupata bao ambalo limekuja kuwa la ushindi, hadi mwisho kijana Michael Mtanga ameweza kuwa bingwa.
Michael Mtanga alikabidhiwa kuku wake jogoo na mmoja wa waratibu wa mashindano hayo Mussa Benjamin, naye mshindi wa pili Charles Chinguile alikabidhiwa mchele kilo tano akiwa kama mshindi wa pili wa mashindano hayo yaliyoanza Jumapili iliyopita kwa kushirikisha watu 18.
Hata hivyo Mratibu msaidizi wa mashindano hayo Mussa Kibichwa amesema kutaanza ligi nyingine ambapo bingwa atapatiwa mchele kilo kumi wakati mshindi wa pili atapewa kilo tano na wa tatu kilo tatu