Yanga yamwandalia mkataba mpya Ngoma

Na Prince Hoza. Dar es Salaam

Mabingwa wa soka nchini, Yanga SC imejipanga kumwongezea mkataba mpya mshambuliaji wake wa kimataifa, raia wa Zimbabwe, Donald Ndombo Ngoma.

Katibu mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema leo kuwa klabu yake imejipanga kumbakiza Ngoma na itampa mkataba mpya.

Mkwasa amedai jukumu hilo la kuhakikisha Ngoma anabaki Yanga na kuondoa uzushi unaozagaa kuwa straika huyo anaenda upande wa pili, Mkwasa ambaye aliwahi kuichezea na kuinoa Yanga miaka iliyopita, amedai Yanga haiko tayari kuona nyota wake wa kikosi cha kwanza wanatoweka.

Juma lililopita, Yanga ilimpoteza kiungo wake wa kutumainiwa, Haruna Niyonzima raia wa Rwanda waliyeshindwana naye huku taarifa zikionyesha kuwa ataelekea upande wa pili baada ya kumtengea mamilioni ya shilingi

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI