Wanyama apewa mtaa Dar

Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam

Kiungo mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs ya Uingereza, Victor Mugubi Wanyama raia wa Kenya, leo amekabidhiwa mtaa wenye jina lake.

Wanyama yupo nchini tangu majuzi na ana ziara ya mapumziko kabla hajarejea kazini Uingereza kwenye timu yake inayoshiriki Ligi Kuu ya Premia, akiwa hapa nchini Wanyama ametembelea maeneo mbalimbali katika jiji la Dar es Salaam.

Leo Wanyama alitembelea Ubungo ambapo alilakiwa na meya wa Manispaa hiyo Boniface Jacob na kutembelea mtaa wa viwandani uliopo Shekilango, kwa heshima, meya Jacob aliamua kuupa jina la Victor Wanyama mtaa wa viwandani.

Kwa maans hiyo Wanyama anakuwa mwanasoka wa kwanza kupewa mtaa kwa hapa nchini, heshima hiyo ni kubwa kwake, pia Wanyama alitembelea Azam Tv ambapo alizungumza na waandishi wa habari

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA