Mtaa wa Wanyama wafutwa
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Watu wasiojulikana wameling' oa bango lililopachikwa rasmi jana na meya wa Ubungo Mhe Boniface Jacob likitambulisha jina la mtaa mpya wa Victor Wanyama Street maeneo ya Ubungo Shekilango.
Victor Wanyama nyota wa Tottenham Hotspurs ya Uingereza ambaye ni raia wa Kenya jana alizuru maeneo hayo ya Shekilango njia na madhumuni kucheki michuano ya Ndondo Cup ndipo alipolakiwa na meya Jacob wa Ubungo.
Meya huyo akaamua kumpa heshima mchezaji huyo wa kimataifa wa Kenya na kuubadili mtaa wa Viwandani jina ambapo akaupa jina la Victor Wanyama na bango likawekwa, lakini haijajulikana ni nani aliyekwenda kung' oa bango hilo