TUNISIA YAICHAKAZA ZIMBABWE 4-1, ALGERIA NAO WATUPWA NJE

Timu ya taifa ya Tunisia imefanikiwa kuingia robo fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika baada ya kuichakaza Zimbabwe mabao 4-1 mchezo wa kundi B mjini Franceville, Gabon.

Mabao ya Naim Slitt, Youssef Msakni, Taha Yassine na Wahbi Khazr yalitosha kabisa kuwapa ushindi huo mnono wakati goli la kufutia machozi la Zimbabwe lilifungwa na Knowledge Musona.

Huo ni ushindi mkubwa kabisa katika fainali hizo za mwaka huu, Ssnegar nao wameifungasha virago Algeria baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 katika mchezo mwingine mkali ambao Algeria wangeweza kuchomoza na ushindi.

Mchezaji wa Leicester City ya Uingereza Islam Sliman alifunga mabao mawili ya Algeria lakini Mousa Sow na Papa Diop wakasawazisha na kuiondosha Algeria mapema kwenye fainali hizo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI