LUFUNGA AIPONZA SIMBA, SASA KUONDOLEWA FA CUP

Na Mrisho Hassan, Dar es Salaam

Kitendo cha Klabu ya Simba kumtumia mchezaji wake Novat Lufunga katika mchezo wake wa kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu kama FA Cup dhidi ya Polisi Dar uliopigwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na Simba kushinda mabao 2-0 umeiponza Klabu hiyo.

Inasemekana Lufunga alionyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wa michuano hiyo mwaka jana dhidi ya Coastal Union hatua ya robo fainali ambapo Simba iliondoshwa kwa kufungwa mabao 2-1, Lufunga alitolewa kwa kadi nyekundu na kwa mujibu wa sheria hakupaswa kucheza katika mchezo wa kwanza wa michuano hiyo inayosimamiwa na TFF na Bodi ya Ligi.

Kwa maana hiyo kamati itakayoketi kuzungumzia sakata hilo inaweza kuiondosha mashindanoni Simba kwa kukiuka kanuni, endapo Simba itaondolewa timu ya Polisi Dar itafuzu hatua ya 16 bora ya mashindano hayo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA