SENEGAR WATINGA ROBO FAINALI AFCON
Senegar imefuzu hatua ya robo fainali ya Mataifa ya Afrika (Afcon) baada ya kuichapa Zimbabwe kwa mabao 2-0.
Mabao ya Senegar yamefungwa na Sadio Mane na Henry Salvet aliyefunga kwa mkwaju wa adhabu. Senegar wangeweza kuibuka na ushindi mnono zaidi lakini umahiri wa kipa wa Zimbabwe ulipunguza mabao ya kufunga.
Kabla katika kundi hilo, Tunisia waliwafunga Algeria kwa mabao 2-1 na kujiweka katika nafasi ya kufuzu. Senegar ina pointi sita ambazo zimeipa nafasi ya kufuzu.
Tunisia inafuatilia ikiwa na pointi tatu, Zimbabwe na Algeria kila moja ina pointi moja na zote zimebakiwa na mchezo mmoja