Mchezaji wa Kagera Sugar afiwa na baba yake
Na Paskal Beatus, Bukoba
Mshambuliaji wa timu ya Kagera Sugar Paul Ngway Ngalyoma amefiwa na baba yake mzazi mzee Lucas Ngalyoma na kumfanya ajiondoe kwenye kikosi hicho ili kushirikiana na familia yake katika msiba huo mkubwa kwake.
Akionyesha masikitiko yake, Nahodha wa Kagera Sugar, George Kavila amesema ni pigo kubwa kwao kumkosa Paul Ngway kwakuwa ameondokewa na baba yake mzazi ambaye amefariki dunia.
"Huo ni msiba wetu sote, mzee Lucas Ngalyoma alikuwa baba wa mwenzetu hivyo sote tumeumia, tunaamini msiba huu umeipata Kagera Sugar nzima kwani tulianza kumkosa Ngway kwenye mchezo wa jana dhidi ya African Lyon" alisema Kavila huku akiwa na huzuni