VAN GAAL AKANUSHA KUSTAAFU UKOCHA
Aliyekuwa meneja wa Man United Louis Van Gaal amesema kuwa hajastaafu na kwamba anachukua likizo ya muda, Van Gaal mwenye umri wa miaka 65 hajajiunga na timu nyingine tangu aondoke Old Trafford mnamo mwezi Mei mwaka jana.
Siku ya Jumatati gazeti moja la Uholanzi De Telegraaf lilisema Van Gaal amemaliza muda wake wa ukufunzi na amestaafu kama mkufunzi hatua iliyoshinikizwa na kifo cha mwanawe.
Lakini alikimbilia kituo kimoja cha redio nchini Uhispania Gadena Ser kwanza ijapokuwa kustaafu kunawezrkana bado hajaamua, Raia huyo wa Uholanzi pia alifichua kwamba amekatas kuifunza Klabu ya Uhispania ya Valencia mwezi uliopita.
"Iwapo nitaendelea au la pia itategemea na maombi nitakayopata", alisema na kuongeza.
"Nimevifunza vilabu vingi na nadhani ni vigumu kuviinua vikiwa katika hali hiyo, sio kweli kwamba nimestaafu, sio sasa, lakini nitaamua mwisho wa likizo yangu mwezi Juni ama Julai mwaka huu", alisema Van Gaal