Olunga afuata mamilioni China

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars Michael Olunga amejiunga na Klabu ya Ligi Kuu ya China Guizhou Hengfeng Zhicheng kwa kitita cha fedha kisichohulikana kutoka kwa Klabu ya Djurgadens IF ya Sweden.

Olunga mwenye umri wa miaka 22 aluachiliwa na Djurgadens IF baada ya vilabu vyote viwili kukubaliana. Kulingana na gazeti la The Standard nchini Kenya, Olunga alikuwa amesalia na miaka mitatu katika kandarasi yake. 

Mchezaji huyo wa zamani wa Gor Mahia na Tusker pua amekuwa akisakwa na Klabu ya Urusi ya CSKA Moscow. Guizhou Zhicheng Hengfeng ilikuwa imemuulizia mshambuliaji huyo na iliripotiwa kuwa tayari kutoa kitita cha shilingi milioni 467 zilizodaiwa na Djugardens..

Olunga pia alikuwa amevutia klabu ya Uturuki ya Galatasaray. Mchezaji huyo aliifungia Gor Mahia mabao 19 katika msimu wa 2015, na kuwasaidia kushinda taji la 15 la KPL pamoja na taji la Top 8 kabla ya kujiunga na klabu hiyo ya Sweden

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA