CAMEROON YATINGA ROBO FAINALI, GABON OUT
Wenyeji Gabon wameondoshwa kwenye michuano ya mataifa ya Afrika baada ya kulazimishwa sare tasa na Cameroon katika mchezo mkali na wa kusisimua.
Licha ya Gabon kumtumainia nyota wakenAubameyang lakini hawakuweza kupata ushindi na kuifanya Cameroon itinge robo fainali kwa kushika nafasi ya pili kwakuwa na pointi tano na hasa baada ya Burkina Faso kuilaza Guinnea Bissau mabao 2-0 katika mchezo mwingine mkali.
Kwa matokeo hayo Burkina Faso wamefikisha pointi tano lakini wanawazidi Cameroon kwa idadi ya magoli ya kufunga, tayari Cameroon imeangukia mkononi mwa Srnegar mchezo ambao unatajwa utakuwa kama fainali kutokana na uimara wa vikosi vyote