Chirwa aisogeza Yanga kileleni
Na Mrisho Hassan, Dar es Salaam
Mshambuliaji wa kimataifa raia wa Zambia Obrey Chirwa leo jioni ameisogeza kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza baada ya kuiongoza Yanga na kuifunga Mwadui FC mabao 2-0 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Hadi mapumziko timu zote zilienda vyumbani zikiwa hazijafungana, Yanga walitengeneza mashambulizi mengi langoni mwa Mwadui lakini umahiri wa kipa wao Shaaban Kado na mabeki wake ulisaidia kupunguza idadi ya mabao.
Kipindi cha pili nacho kilionekana kigumu kwa timu zote, Lakini Obrey Chirwa aliyeingia kuchukua nafasi ya Mnyarwanda Haruna Niyonzima alipachika mabao yote mawili yalioipa Yanga ushindi huo wa mabao mawili yaliyoiweka kileleni.
Yanga sasa ndio vinara wa Ligi hiyo wakiipoka Simba ambayo jana ililala dhidi ya Azam ikifungwa 1-0, Yanga wana pointi 46 sasa ikiwa imeiacha Simba kwa tofauti ya pointi moja zote zikishuka dimbani mara 20