Mchezaji wa zamani wa Simba na Yanga ahukumiwa kifungo
Na Mwandishi Wetu
Mchezaji wa zamani wa Tukuyu Star, Ndovu ya Arusha, Yanga na Simba Seleman Mathew Luwongo amehukumiwa kifungo cha kwenda jela miezi 6 bila kulipa faini yoyote baada ya kufanya mkutano wa kisiasa wa hadhara bila ya kibari.
Taarifa ambazo Mambo Uwanjani inazo zinasema kuwa Mathew ambaye aliwahi kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amefanya mkutano wa kisiasa akiwa na chama.chake kipya cha CHADEMA mkoani Lindi ambako anakoendesha shughuri sake za kisiasa.
Serikali ya Awamu ya tank inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli imepiga marufuku mikusanyiko yote ya kisiasa bila kupata kibari maalum, lakini Mathew na wenzake walikiuka agizo hilo na kujikuta akianzia mwaka 2017 gerezani