Ivory Coast yanusurika kichapo Afcon
Mabingwa watetezi wa Mataifa ya Afrika, Ivory Coast wamenusurika kichapo kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kufungana mabao 2-2 na DR Congo mechi ikipigwa katika Uwanja wa Stade d'Oyen Libraville Gabon.
DR Congo ilitangulia kupata bao la kuongoza kunako dakika ya 9 lililofungwa na Kabano kabla ya Wilfred Bony kuisawazishia Ivory Coast katika dakika ya 26 kipindi cha kwanza.
Mshambuliaji hatari wa DR Congo Kabananga alipachika bao la pili katika dakika ya 28, hadi mapumziko DR Congo ilikuwa ikiongoza kwa mabao hayo mawili kwa moja.
Mabingwa watetezi Ivory Coast walisawazisha bao katika dakika ya 67 kipindi cha pili likifungwa na Die na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare, lakini katika mchezo mwingine Morocco iliichabanga Togo mabao 3-1