Adebayor apata timu Uturuki

Mshambuliaji wa kimataifa raia wa Togo Emmanuel Adebayor amejiunga na timu ya Ligi Kuu nchini Uturuki ya Istanbul Basaksehir ambayo kwa sasa inakamata nafasi ya pili.

Adebayor amesaini mkataba wa miezi 18 huku kiasi cha pesa alichokabidhiwa ni siri kati yao, Nyota huyo sliyekuwa na timu yake ya taifa ya Togo kwenye fainali za mataifa Afrika nchini Gabon na kuondoshwa mapema ikiwa ya mwisho kwenye kundi C sasa ataanza maisha mapya Uturuki.

Bosi wa timu hiyo Mustafa Erogut amesema walikuwa wakimtaka Adebayor kwa kipindi kirefu hivyo kumpata sasa imekuwa furaha kwao na wanaamini Adebayor atawafaa.

Adebayor aliwahi kuzichezea Klabu za Arsenal, Manchester City, Tottenham Hotspur za England na Real Madrid ya Hispania

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA