Ferguson amfagilia Mourinho
Manchester United wanaendelea kuimarika chini ya meneja Jose Mourinho na ni bahati tu wamekosa lakini wangekuwa wakikabiliana vilivyo na Chelsea amesema meneja wa zamani Sir Alex Ferguson.
Ferguson (75) alistaafu kams meneja mwaka 2013 lakini bado ana uhusiano wa karibu na Klabu hiyo ya Old Trafford kwani huhudhuria michezo yao mingi, "Nafikiri Mourinho amefanya kazi kubwa" amesema Ferguson katika mahojiano yake na BBC Sports.
Ferguson pia alielezea kwa nini rekodi ya ufungaji magoli ya mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney haitavunjwa na mchezaji yoyote yule karibuni.
Jose Mourinho ni meneja wa tatu kuiongoza Klabu ya Manchester United tangu Ferguson kustaafu alipochukua nafasi ya Louis Van Gaal mwezi Mei.
Ingawa Mourinho alishinda mechi tatu zake za kwanza akiwa Manchester United, alishinda alama sita pekee kutoka kwa mechi saba za Ligi ya Premia zilizofuata