Wasweden wa Ulimwengu wamnasa Ndemla
Na Salum Fikiri Jr, Dar es Salaam
Klabu ya AFC Eskilstuna inayoshiriki Ligi Kuu ya Sweden imethibitisha kufanya mazungumzo na Klabu ya Simba ya Tanzania ikitaka kumsajili kiungo mshambuliaji wa Simba Said Khamis Ndemla.
AFC Eskilstuna ndiyo iliyomsajili Mtanzania mwingine Thomas Emmanuel Ulimwengu kwa mkataba wa miaka mitatu imevutiwa na Ndemla ambaye kwa sasa si chaguo la kwanza kwenye kikosi hicho kinachonolewa na Mcameroon Joseph Marius Omog.
Mmoja wa mabosi wa timu hiyo iliyopanda Ligi Kuu msimu huu Hans Joachim Watkze amesema wanataka kumsajili Ndemla ambaye wamevutiwa naye na tayari wameshafanya mazungumzo na uongozi wa Simba ili waweze kumnasa.
Hata hivyo Simba hawajaonyesha nia ya kumwachia licha kwamba wamekuwa wakimtumia Ndemla kama mchezaji wa akiba