Simba nao waikacha Mamelodi

Na Ikram Khamees, Dar es Sakaam

Simba SC nao wametangaza kuikacha Mamelodi Sundows ya Afrika Kusini ambayo ilikuwa wacheze nayo kesho Jumatano katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mchezo wa kirafiki.

Mamelodi wamewasili nchini ambapo ziara yao imeratibiwa na Rahim Zamunda Kangezi ambaye ni mmiliki wa timu ya Ligi Kuu Bara African Lyon na ilikuwa icheze mechi mbili na Yanga na Simba.

Mamelodi imeletwa kwa kampeni maalum ya kupinga ujangili wa tembo hivyo sasa italazimika kucheza mechi moja na Azam FC katika uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Meneja wa Simba Mussa Hassan Mgosi amesema wameamua kuikacha Mamelodi kutokana na kukabiliwa na ushindani mkubwa kwenye mechi za Ligi na hivyo wanaogopa majeruhi kwani mchezo wao na Mamelodi ungekuwa mgumu kwakuwa Mamelodi ni mabingwa wa Afrika.

Mgosi ameongeza kuwa kocha wao Mcameroon Joseph Omog amwasilisha mapendekezo yake na kuona ni bora Simba ikaachana na mchezo huo wa kirafiki ambao ungefanyika kesho, Simba itasafiri Alhamisi kuelekea Songea ambapo Jumamosi itacheza na Majimaji

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA