Mkwasa awa katibu mkuu Yanga
Na Salum Fikiri Jr, Dar es Salaam
Aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ameteuliwa kuwa katibu mkuu wa Klabu ya Yanga leo na ataanza rasmi majukumu yake kesho.
Makamu mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga amesema, Mkwasa anakuwa katibu mkuu akichukua mikoba ya kaimu katibu mkuu Baraka Deusdetit ambaye amerejeshwa kuwa Mkurugenzi wa fedha.
Mkwasa aliyewahi pia kuichezea Yanga na baadaye kuifundisha, amekubali kuchukua cheo hicho na ameahidi kuifanyia makubwa Yanga, wengi wameshangazwa na uteuzi huo kwani wamezoea kumuona Mkwasa akiwa kama kocha.
Lakini Sanga amesema Mkwasa anao uwezo wa kuiongoza Yanga kama katibu kwani anayo elimu ya kutosha, Mkwasa anaye amedai hatoingilia kazi za benchi la ufundi na atafanya kile kilichompeleka, Mkwasa alikuwa kocha wa Taifa Stars akirithi mikoba ya Mholanzi Mart Nooij